7 Oktoba 2020 - 11:19
Ushindi mwingine wa Maduro baada ya Mahakama ya Rufaa ya Uingereza kutoa hukumu kwa maslahi ya Venezuela

Tangu kuanza mgogoro wa uchaguzi nchini Venezuela, Umoja wa Ulaya na nchi kubwa za Ulaya zimechukua msimamo sawa na wa Marekani dhidi ya Rais Nicolas Maduro wa Venezuela. Baada ya kinara wa wapianzani, Juan Guaido kushindwa katika uchaguzi na kisha kujitangaza rais mnamo Januari 23, 2029, nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza, zimekuwa zikimuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Nchi hizo zilichukua hatua kadhaa za kumuunga mkono lakini hatimaye hatua hizo zimegonga mwamba na kutofanikiwa. Mahakama ya Rufaa ya Uingereza hivi karibuni ilibatilisha hukumu ya mahakama ya nchini humo ambayo imekuwa ikimtambua kinara wa upinzani Juan Guaido kuwa rais wa Venezuela na kutaka akabidhiwe dhabu ya Venezuela yenye thamani ya dola bilioni moja. Miezi kadhaa iliyopita, Mahakama Kuu ya Uingereza, kwa kutegemea uamuzi wa London kumtambua Juan Guaido kama rais wa Venezuela, ilitaka akabidhiwe dhahabu hiyo. Majaji wa Mahakama ya Rufaa ya Uingereza wamesema yamkini taarifa ya serikali ya Uingereza kumhusu Juan Guaido haiakisi uhalisia wa mambo huko Venezuela. Jaji Stephen Males, mkuu wa jopo la majaji katika mahakama hiyo amesema hatua ya Uingereza ya kumtambua rasmi Guaido imejaa utata.

Baada ya Marekani kumtambua Guaido kama rais wa kisheria wa Venezuela, zaidi ya nchi 10 za Ulaya ikiwemo Uingereza mnamo Februari 4 2019 zilichukua hatua isiyo ya kisheria na kumtambua Juan Guaido kama 'rais wa muda wa Venezuela'. Aidha nchi hizo za Ulaya zilisema Nicolas Maduro ambaye alichaguliwa kwa wingi wa kura kuendelea kuwa rais wa Venezuela ni rais aliyeko madakrani kinyume cha sheria. Kufuatia maamuzi hayo, si tu kuwa nchi za Ulaya zilianza kutekeleza kila aina ya vikwazo dhidi ya Venezela ili kuiangusha serikali halali ya Maduri, bali pia zilichukua hatua kadhaa ili kuhakikisha kuwa Juan Guaido anaingia madarakani kama rais wa Venezuela. Nchi hizo zilianza kutambua na kuwakaribisha katika nchi hizo wawakilishi wa Guaido. Aidha kulianzishwa jitihada za kutumia vyombo vya sheria kuzuia mali za Venezuela katika nchi hizo za Ulaya na kuzikabidhi kwa Guaido na timu yake.

Juan Carlos Idealgu mtaalamu wa masuala ya kisiasa katika Amerika ya Latini  anasema mpango wa kumpindua Nicolas Maduro haukuzingatia uhalisia wa mambo.

Pamoja na kuwepo njama hizo za Ulaya na Marekani lakini Umoja wa Mataifa unaendelea kuitambua serikali ya Maduro kama serikali ya kisheria Venezuela. Kwa msingi huo njama za Marekani na washirika wake wa Ulaya dhidi ya Venezuela zimegonga mwamba kwa sababu hazikuwa na msingi wa kisheria.

Ni kwa kuzingatia nukta hiyo ndiposa Mahakama ya Rufaa ya Uingereza ikasaema dhahabu ya Venezuela ikabidhiwe serikali halali ya nchi hiyo. Hukumu hiyo inahesbiwa kuwa ushindi mkubwa kwa serikali ya Venezuela na Maduro. Mbali na umuhimu wa kifedha na kiuchumu wa hukumu hiyo, kadhia muhimu zaidi ni kuwa, Mahakama ya Rufaa ya Uingereza imeshindwa kufumbia macho ukweli ulio wazi ambao ni kuwa, serikali halali ya Venezuela inaongozwa na Nicolas Maduro. Kwa hivyo hukumu hiyo ni ushindi mkubwa kwa Maduro na pigo kubwa kwa serikali ya Donald Trump na washirika wake barani Ulaya ambao wamefanya kila wawezalo kumdhoofisha Maduro.

Mwezi Mei mwaka 2018, watu wa Venezuela walipiga kura katika uchaguzi huru na wa wazi ambapo kupitia asilimia 68 ya kura zote walimchagua tena Madurio kuiongoza nchi hiyo. Kwa hivyo hatua ambazo zilichukuliwa na Marekani na washirika wake wa Ulaya hazikuwa tu ni uingiliaji wa wazi na ulio kinyume cha sheria katika masuala ya ndani ya Venezuela bali hatua hizo zilikuwa kinyume cha chaguo la watu wa nchi hiyo ya Amerika ya Latini. Wamagharibi wamekuwa wakifanya juu chini kumuingiza Guaido madarakani kwa kutumia mashinikizo ya kisiasa, kiuchumi na hata kijeshi ili waweze kufikia malengo yao haramu nchini Venezuela.

342/